Tuesday 9 February 2010

UKIMWI BADO GUMZO KWA WANZANZIBARI

Licha ya kutolewa elimu ya kutosha kuhusu ukimwi kwa wananchi wa Zanibar kwaUnguja na Pemba, lakini bado jamii haionekani kukubaliana na elimu wanayopewa.

Hivi karibuni nilitembelea sehemu mbali mbali za mjini Unguja katika pita pita yangu nilikutana na kikundi cha vijana wasiopungua watano na miaka yao kati ya 21 na kuendelea, walinishangaza kwa kile wanachozungumza.

Wanazungumzia UKIMWI lakini kwa nyanja tofauti, wanamzungumzia kijana mwenzao ambae amegundulika na maradhi hayo ambapo wanajadili jinsi gani watakaa nae manaake ametenda dhambi kubwa mbele ya Mungu na jamii iliyomzunguka.

Niliwauliza kwanini wanafikiria hivyo? walinijibu hujui kama ukiwa na ukimwi ni muhuni! na wao hawawezi kukaa na muhuni kwani nawao wataonekana ni wahuni kama yeye.

Ilinisikitisha kusikia hayo kwani nilikuwa nnakotoka kabla ya kukutana na vijana hao niliupata mkasa wa mtoto anaelelewa na bibi yake kwasasa na amekosa wa kucheza nae mtaani hapo kisa anaishi na virusi vya ukimwi alivyoambukizwa na wazazi wake, na baadhi wazee wa mtaa huwakataza watoto wao kutocheza na mtoto huyo kwakuwa ana ukimwi.

Ilinisikitisha kwani wanofanya unyanyapaa huo ni watu wazima ambao wao wenyewe hatma yao hawaijui! Na kwa upande mwengine hata huyo mtoto anaefanyiwa unyanyapaa huo, haujui hata huo ukimwi kwani ndio kwanza ana umri wa miaka minne. Ukweli ni kwamba machozi yalinitoka nilipomuona huyo mtoto wenyewe na jinsi anavyofanyiwa ni huruma kweli.

Turudi katika hadithi yetu,kwa kuwa nawajuwa vijana wale wanaomhadithia mwenziwao ameambukizwa nilisogea karibu nao nikawauliza kama ifuatavyo. "Asalam Alaykum wakaitikia vizuri " Aleykum Msalaam, nikawauliza kwanini wanasema hivyo? Na hili ndilo jibu lao....... Ukiwa na ukimwi lazima utakuwa muhuni na hasa katika masuala ya ngono kwaiyo tunafanya hivyo ili nasisi tusije kuonekana kama yeye.

Mmmmhhhh huo ni mguno ulionitoka baada ya kupata maelezo kwani nilijua kumbe bado kazi ipo ya kutoa elimu inayohusu UKIMWI baada ya hapo niliwauliza tena, kwanini wanafikiria hivyo?na walinijibu kuwa.... hakuna njia au sababu ya kupata ukimwi ikiwa si muhuni na rafiki yao huyo lazima ni muhuni ndio maana ameambukizwa. Sijaamini nilichokisikia kutoka kwa vijana hao lakini ndio hali halisi ilivyokuwa.

Ukweli ni kwamba nilichukuwa muda kuwafamisha mpaka nikautoa mkasa wamtotoyule malaika wa mungu ambaye hata zinaa haijui na watu kama wao hawataki kumbeba,kucheza nae na hata kuthubutu kuwakataza watoto wao, je mtoto huyo amezini lini au huo uhuni wanaosema ameufanya lini? Hapo ndipo waliponielewa kwani mpaka baadhi yao wakadondosha machozi.

Hao ni baadhi yao lakini kunawengine huwa na uthubutu ya hata kuwakataa na kuwafukuza majumbani mwao ndugu, jamaa na marafiki pale wanapokundua kuwa wanaishi na VVU.

Vilevile kumekuwa na wagonjwa wa UKIMWI wanaotelekezwa hospitali bila ya huduma yoyote kutoka katika familia yake na hata mauti yakimfikia basi hakuna uthubutu nani atakaekwenda kumstiri kisa anaukimwi hiii inatokea katika visiwa hivi, ambapo asilimia kubwa ya wananchi wake wanao ufahamu wa nini UKIMWI.

Nini kifanyike kuidhibiti hali hii? ikiwa elimu juu ya ukimwi bado inatolewa!

Kwa upande wangu sitokata tamaa ya kumuelewesha mtu yoyote ambae nikimuona ana mawazo kama niliyowakuta kwa vijana hawa niliokuhadithia lakini mpaka lini wanzanibari tutakuwa hivi? Ikiwa mzazi uneiyongoza familia yako unamtenga mwanao alieambukizwa na unamkataza mwanao asieambukizwa kushirikiana na alie ambukizwa, je wewe ushaijua hatma yako na ya yule unaemchunga?

No comments:

Post a Comment