Thursday 11 February 2010

Abdulrazak Gurnah kutoka ukimbizi hadi uprofesa nchini UK

Kujitokeza kwa vijana wingi kukimbilia nchi za nje kwa lengo la kutafuta maisha,kumbe ni muendelezo wa kile kilichoanzwa na wazazi wao miaka mingi iliopita.

Ninapomtaja Abdulrazak Gurnah ambae ni mzaliwa wa Zanzibar miaka 62 iliyopita ni kati ya wanzanzibari wa mwanzo ambao waliamua kwenda kuyawekeza maisha yao nchi za nje na yeye alielekea Uingereza miaka minne baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwanini aliamua kwenda huko? Katika tovuti yake Abdulrazak Gumnah anasema sio rahisi kukabiliana nacho kile kilichomkuta,anasema alikutwa na misukosuko mingi ikiwa kujiingiza katika maisha ya ukimbizi,ubaguzi wa rangi pamoja na kukosa haki za kimsingI.

Gurnah ambae amezaliwa mwaka 1948 Zanzibar kwa sasa ni mkufunzi wa lugha katika chuo cha Kent nchini London, na mwenye familia inayomtegemea wakiwemo watoto na mke,amefikia hatua hiyo baada ya kutokata tamaa na aliweza kujisomesha hadi kfikia hapo alipo kwa sasa, na mnamo miaka ya 1980 hadi 1982 alipata nafasi ya kuwa mwalimu katika chuo cha Kano nchini Nigeria.

Pr.Gurnah kwa sasa mhariri katika gazeti la linajulikana la wasafiri linalochapishwa nchini Uingereza.

Vilevile Pr. Gurnah ni muandishi mwa vitabu na ameshawahi kuwandika vitabu saba,ambapo vitatu kati vimempatia umaarufu navyo ni Paradize,Desertion na By the Sea vyote hivi ameviandika kulingana na mazingira aliyopitia hadi kufikia uprofesa.

chanzo cha habari ni http://www.abdulrazak%20gurnah/

No comments:

Post a Comment